Baada ya
pambano la karne kufanyika na matokeo kuwa mazuri kwa Floyd Mayweather
swali aliloulizwa baada ya pambano ni kwamba atakuwa na pambano lingine
akasema "yes, mwezi wa tisa ana pambano". Baada ya hapo alivyokuwa kwenye
press conference alivyoulizwa nani utamtaka kwa ajili ya pambano lako la
mwisho mwezi wa tisa. Mayweather alijibu kwa kifupi “Khan”.
Amir Khan
ni bondia kutoka England ambaye na yeye ni bondia maarufu na mara nyingi
amehusishwa kuhusu pambano kati yake na Mayweather. Pambano hilo ndio
litakuwa la mwisho kwa Money Money. “Baada ya pambano langu la mwezi wa
tisa nitastaafu kucheza tena boxing”.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni