Polisi
mjini Texas wanasema kuwa wamewapiga risasi na kuwaua watu wawili
waliokuwa na silaha, waliowashambulia walinda usalama kwa risasi,
walipofika katika eneo la hafla moja yenye utata ya uchoraji wa vibonzo
vya kuwakejeli waislamu na mtume Mohammad.
Duru za habari zasema
kuwa kisa cha ushambuliaji wa risasi kimefanyika katika sherehe moja,
iliyokuwa ikifanyika mjini Dallas, mahala ambapo waandalizi walikuwa
wakiendesha onesho hilo.Hafla za Sherehe hiyo iliyoandaliwa na kundi moja la kisiasa la kihafidhina, ambalo limekuwa likikejeli Uislamu, lilikuwa litoe zawadi nono ya dola milioni kumi kwa mchoraji kibonzo mahiri zaidi, atakayeibuka mshindi kwa kumchora mtume Mohamad.
Mwanasiasa kutoka Uholanzi Geert Wilders -- ambaye anafahamika kwa matamshi yake ya kuwadunisha waislamu, alikuwa msemaji mkuu katika hafla hiyo.
Aliyeshuhudia tukio hilo ameiambia BBC kuwa, aliwaona maafisa wa polisi wakimtia mbaroni mshukiwa wa tatu, ambaye alionekana kuwa hana silaha.
Kikosi cha kutegua mabomu pamoja na helikopta za polisi zimefika mahali hapo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni