Elisha Waziri, mkazi wa Kimara-Mwisho akizungumza na mwanahabari wa Global TV Online, Melkiadi Oreje.
Kwa mara
nyingine mgomo wa mabasi yaendayo mikoani na mabasi madogo (daladala)
jijini Dar umeibuka na miji mingi nchini kumewafanya wananchi watumiao usafiri huo kubaki
katika hali ya sintofahamu kwa kushindwa kufanya shughuli zao za kila
siku.
Mgomo huo
umechukua sura mpya baada ya madereva kudai kuwa serikali imekiuka
ahadi waliyopewa na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka kuwa
hawatasoma kila baada ya miaka mitatu pindi wanapotaka kuhuisha leseni
zao.
Mbali na
madai hayo, madereva hao wameweka mgomo kwa kigezo cha kushinikiza
waajiri wao wawape mikataba ya kudumu. Mwandishi wetu amezunguka maeneo
mbalimbali ya Jiji la Dar na kujionea hali halisi ya mgomo wa mabasi ya
mikoani pamoja na daladala zikiwa hazifanyi kazi.
Mwanahabari
wetu aliyeambatana na Timu wanahabari wa Global TV Online, alifika eneo
la Stendi ya Kimara-Mwisho na kukuta wananchi wakitumia usafiri
bodaboda na Bajaj kwenda katika sehemu zao za kazi huku baadhi yao
wakieleza usumbufu mkubwa walioupata kutokana na mgomo huo.
“Kimsingi
sisi wananchi mgomo huu unatuumiza zaidi. Mimi nafikiri wahusika wa
pande zote mbili wanapaswa kuchukua hatua za haraka ili kutunusuru sisi
tunaotumia usafiri huu lakini pia uzalishaji wa taifa,” alisema Juma,
mkazi wa Kimara-Mwisho.
Aidha wananchi wanashauriwa kuanza mazoea ya kutembea kwa miguu pale ambapo hawaendi mbali kama sehemu pia ya kujenga afya zao
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni