Waziri
mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ameelezea mshangao wake binafsi kwa
mwanajeshi wa Israeli wa asili ya Ethiopia ambaye alipigwa na polisi wa
Israeli hali iliyosababisha kutokea kwa maandamano.
Bwana Netanyahu alimuambia Damas Fikadeh kuwa kitendo hicho hakikubaliki, na madabiliko yanahitaji kufanywa.Bwana Fikadeh alisema alitiwa moyo na matamshi yake waziri mkuu na ni wakati wa kumaliza ghasia za ubaguzi dhidi ya Waisraeli wa asili ya Ethiopia.
Wakati wa ghasi hizo za siku ya jumamosi usiku mjini Tel Aviv takriban watu 50 walijeruhiwa.
Wakati huohuo rais wa Israeli Reuven Rivlin amesema kuwa ni makosa jinsi Israeli inavyowafanyia wayahudi wenye asili ya Ethiopia.
Akizungumza baada ya maandamano yenye ghasia mjini Tel Aviv bwana Rivlin alisema kuwa kidonda kilicho wazi kimeonekana nchini Israeli, lakini ghasia sio suluhu.
Zaidi ya watu 50 walijeruhiwa siku ya Jumapili wakati polisi wakitumia vitoa machozi kuwatawanya mamia ya waandamanaji
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni