Polisi 12 wamekamatwa nchini Malaysia kufuatia tuhuma za kushirikiana na walanguzi wa binadamu.
Waziri
wa maswala ya usalama wa ndani Wan Junaidi Tuanku Jaafar amesema wawili
kati ya maafisa hao 12 wamehusishwa na usafirishaji wa wahamiaji.Waziri huyo pia amekariri kuwa makaburi 139 yaliyogunduliwa karibu na mpaka wa Thailand majuzi, hayakuwa ya halaiki.
Eneo yalikogunduliwa makaburi hayo ndio mapito yanayotumika na walanguzi wa binadamu kuwasafirisha wahamiaji kutoka Myanmar na Bangladesh kuingia Malaysia.
Asilimia kubwa ya wahamiaji hao ni wa kutoka jamii ya waislamu wa Rohingya wanaotoroka hujuma nchini Myanmar
Katika siku za hivi karibuni maelfu ya raia wa Bangladeshi pia wameanza kutoroka umaskini uliokithiri nchini mwao.
Bwana Wan Junaidi aliwaambia waandishi wa habari kuwa wawili kati ya maafisa wa polisi waliokamatwa wanahusika moja kwa moja na makaburi ya '' Wang Kelian".
Maafisa wa utawala wanaamini kuwa asilimia kubwa ya makaburi hayo yanamabaki ya wahamiaji.
Wakati huohuo Kiongozi wa kidini wa Tibet Dalai Lama, amemuomba mwenzake mshindi wa tuzo ya amani, Aung San Suu Kyi, kufanya jitihada zaidi ili kuwasaidia watu wa jamii ya Rohingyas Nchini mwake na huko Myanmar.
Katika uchambuzi wa magazeti na Muaustralia huyo, Dalai Lama alisema kwamba awali aliwahi kutoa maelezo kama hayo kwa Bi Suu Kyi,
huku akizidi kuwa na matumaini kuwa ana uwezo wa kushughulikia swala hilo.
Mshindi huyo wa tuzo ya Nobel anakosolewa kote Duniani kwa kukataa kuzungumzia swala hilo la watu hao wa kabila la Rohingya, ambao hawatambuliwi kama raia
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni