Tembo
wakiwa wamemzunguka mwenzao kumpatia msaada. SUALA la umoja si kwa
wanadamu pekee bali hata wanyama kama tembo nao wanao umoja miongoni
mwao.
Katika
tukio lililonaswa kwenye video huko nchini Afrika Kusini na kuwekwa
kwenye mtandao wa Youtube linawaonyesha tembo walioamua kufunga barabara
na kusababisha foleni ya magari ili wamuokoe mwenzao aliyedondoka
katikati ya barabara hiyo.
Tembo
huyo akiwa chini baada ya kudondoka.Tembo huyo mdogo alidondoka wakati
akitembea barabarani kwenye Hifadhi ya Taifa ya Kruger iliyopo Afrika
Kusini. Baada ya tukio hilo tembo wakubwa walikuja na kufunga barabara ili kumpatia msaada mwenzao huyo.
Tembo
huyo akijaribu kuinuka kwa msaada wa wenzake. Baada ya kuangaika kwa
muda, tembo huyo mdogo alifanikiwa kusimama kwa msaada wa wenzake na
kuendelea na safari ambapo wenzake nao waliamua kutoka barabarani na
kuwafanya madereva wa magari kuendelea na safari zao.
...Hatimaye tembo huyo akafanikiwa kuinuka.
...Akitokomea na wenzake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni