Askari
mmoja ameripotiwa kujeruhiwa baada ya kuwepo kwa mapambano makali kati
ya Polisi na Wanamgambo wa Al Shabaab Kaskazini Mashariki mwa Kenya
Wizara ya usalama wa Taifa nchini Kenya imethibitisha kuwa askari mmoja
amejeruhiwa wakati wa shambulizi la Wanamgambo wa al shabaab katika
kijiji cha Yumbis mjini Garissa, Kaskazini Mashariki mwa Kenya. Msemaji
wa wizara hiyo Mwenda Njoka ameiambia BBC kuwa kulikuwa na makabiliano
makali kati ya Polisi na wapiganaji hao.Viongozi katika eneo hilo wamesema Magari manne ya Polisi yamechomwa moto na wanamgambo. Polisi wameiambia BBC kuwa wamepeleka kikosi kuimarisha hali ya usalama.
Taarifa za awali zilieleza kuwa askari kadhaa wanahofiwa kufa kwenye kwenye shambulio la usiku wa jumatatu.
Wakati huo huo al shabaab wamedai kuhusika katika shambulio hilo wakidai kuwa wamewaua Polisi 20, lakini vyombo vya usalama vimesema madai hayo ni Propaganda.
Siku ya jumatatu Polisi watatu walijeruhiwa baada ya Gari lao kukanyaga Bomu la kutegwa ardhini.
Kikosi cha askari 20 kilifika katika eneo hilo kuwasaidia waliojeruhiwa wanaoelezwa kushambuliwa na Al Shabaab.
Al shabaab wamekiri kuhusika katika shambulio hilo na kuchoma magari mjini Garissa. Msemaji wa kundi hilo Shaykh Abdiasis Abu Mus’ab amesema shambulio hilo limefanywa na kikosi maalum kiitwacho ‘mujahidin’.
Mus’ab amesema shambulio lilikuwa la “mafanikio” na kudai kuwa hasara waliyoipata askari wa Kenya ni kubwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni