Mwana
wa mfalme wa Uingereza, Prince William ametoa wito kwa shirikisho la
soka duniani FIFA kuweka maslahi ya soka mbele ya matamanio ya
kibinafsi.
Kwenye hotuba yake kabla ya fainali ya kombe la FA
nchini Uingereza, William ambaye pia ni rais wa shirikisho la soka la FA
nchini Uingereza, ameilinganisha sakata ya FIFA na ile ya jiji la
Salt Lake ilivyofanyika wakati Marekani ilikuwa inasaka tiketi ya
kuandaa mashindano ya olimpiki ya barafu mnamo mwaka wa 2002 na
kuilazimu kamati ya kimataifa ya Olimpiki kuimarika."Inaonekana kuna mgawanyiko mkubwa kati ya wanaocheza na kushabikia mchezo huo na madai ya ufisadi yanayowakabili wasimamizi wa mchezo huo. Alisema"
"Matukio ya Zurich wiki hii yanasadifiana na wakati wa Salt Lake ambapo kamati ya Olimpiki, IOC ilipitia hali kama hii ya FIFA.
''Sawa na IOC inastahili kuonesha ina uwezo wa kujali maslahi ya mchezo huo".
Wakati huo huo, Mamlaka ya Uswizi, imeanzisha uchunguzi zaidi kuhusu utoaji wa ruhusa ya uwenyeji wa mashindano ya kombe la dunia mwaka wa 2018 na 2022 kwa mataifa ya Urusi na Qatar mtawalia.
Mwanamfalme William ndiye aliyeiongoza kamati ya Uingereza ya kuwania uwenyeji wa kombe la dunia la 2018 akiwa pamoja na mchezaji wa zamani wa Uingereza, David Beckham.
"Wanaounga mkono FIFA wakiwemo wadhamini na mashirika ya jumuiya, wanastahili kuchukua jukumu la ya kushinikiza mabadiliko ndani ya FIFA".
''Iwapo hatutafanya hivyo, tutakuwa hatuwatendei haki wapenzi wa mchezo huo na mchezo wasoka kwa jumla".
Kando na hayo, Mwenyekiti wa FA, Greg Dyke, amesema kuwa Uingereza iko tayari kuunga mkono hatua ya shirikisho la soka barani ulaya UEFA kususia kombe la dunia la 2018.
Wasimamizi wa soka barani Uropa wanapanga kukutana jijini Berlin wiki ijayo kufanya maamuzi ya iwapo watasusia mchuano wa kombe la dunia la mwaka wa 2018 utakaoandaliwa Urusi au la
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni