Aliyekuwa mlinzi wa timu ya Uingereza na Klabu ya Manchester United, Rio Ferdinand amestaafu kucheza kandanda ya kulipwa.
Ferdinand
amesema kupitia kwa taarifa kwa meza ya michezo ya BT kuwa anahisi
wakati umewadia kwake kufunganya virago na kushabikia mchezo anaoupenda.Hatua hiyo ya mlinzi hiyo inafuatia kuruhusiwa kwake kuondoka na klabu ya Queens Park Rangers.
Klabu hiyo ya QPR ilimruhusu kuondoka baada ya kushushwa daraja baada ya kumaliza katika nafasi ya 20 katika ligi ya msimu huu iliyokamilika juma lililopita.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 amesema ''nafikiri huu ndio wakati wa kustaafu kutoka kwenye mchezo ninaopenda''
''Lakini najivunia kuiwakilisha taifa langu katika mechi 81 za kimataifa'
“Ningependa
kutoa shukrani zangu za dhati kwa Chris Ramsey, Harry Redknapp, David
O’Leary na David Moyes ambao waliniwezesha katika nyakati tofauti katika
maisha yangu ya soka bila ya kusahau wafanyakazi wengine katika timu
ambao walionyesha kunijali kwa miaka yote. Pia wachezaji wote ambao
nimewahi kucheza nao. Ningependa kutoa shukrani kwa timu iliyonisaidia
wakati nikiwa nje ya mchezo huu, Jamie Moralee na kila mtu katika
kipindi hiki kipya ninachokianza rasmi.”
“Kushinda
makombe kwa kipindi cha miaka 13 nikiwa na klabu ya Manchester United
ilinifanya nifanikiwe kila kitu nilichokuwa nikikitamani katika tasnia
ya soka. Tangu utotoni mpaka wakati huu, hicho ndicho nilichokuwa
nikikiwaza mara zote. Vyote hivyo sidhani kama vingewezekana bila ya
kiungo muhimu kabisa ambaye ni, Sir Alex Ferguson. Upeo wake mkubwa
katika macho yangu utaendelea kudumu daima. Kwa mtazamo wangu yeye ndiye
atabaki kuwa kocha bora kabisa katika historia ya mpira wa Uingereza.”
“Pia
ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa mke wangu Rebecca na
familia yangu, akiwemo mama na baba yangu kwa kujitolea maisha yote juu
yangu pia faraja na ushauri wao waliokuwa wakinipa kwa kipindi chote
nilichokuwa nikisakata soka”
“Na
mwisho kabisa, ningependa kuwashukuru mashabiki wote katika klabu zote
kwani bila yao mpira huu uliojaa utaalamu wa hali juu usingekuwepo.
Nitamkumbuka kila mmoja wenu kwenye jioni hii ya siku ya Jumamosi.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni