Jumanne, 26 Mei 2015

VITU 5 VILIVYOPIGA MARUKUA DUNIANI LAKINI TZ RUKSA

Nimekusanya list ya vitu 5 ambavyo kwa nchi za wenzetu kama Marekani, Ujerumani, Hispania, Ufaransa na Bangladesh pamoja na sehemu nyingine duniani ni vitu ambavyo kisheria vimepigwa marufuku lakini kwa huku kwetu ni halali kabisa kutumika.

Hii hapa list ya vitu hivyo.
1. Baby Walker

Mwaka 2004 Canada ilipitisha sheria ya kukataza Baby walkers ndani ya nchi hiyo wakidai kwamba mtoto akitumia baby walker anachelewe kutembea na pia kudumaza akili. Mtu yoyote atakayekutwa anamiliki au ananunua kifaa hicho faini ni dola 100,000 au kifungo cha miezi 6 jela.
2. Tomato Sauce #HeinzKetchup

Kama ulihisi Tomato Sauce zote ni ruksa kila sehemu basi jibu ni hapana. Mwaka 2011 tomato sauce ya ‘HEINZ TOMATO KETCHUP’ ilikatazwa kutumika kwenye Kanteen za shule Ufaransa na pia ilikatazwa kusafirishwa kwa baadhi ya nchi za Ulaya.

3. Mifuko ya Rambo.

Nchi ya kwanza kukataza mifuko ya rambo kutumika ni Bangladesh kwa sheria iliyopitishwa huko mwaka 2002.. California nako walipitisha Sheria hiyo mwaka 2012-13 na mpaka sasa hakuna sehemu utaenda California alafu ukawekewa kitu kwenye mfuko wa rambo.
4. Big g

Mwaka 1992 Singapore ilipitisha sheria iliyokataza kuuza ama kusafirisha big g kwa nchi yoyote duniani, ila big g zitengenezwe kwa ajili ya kulika na kununuliwa na raia wa Singapore tu. Baada ya miaka 12 yalifanyika mabadiliko na kuruhusu watu wa Singapore kununua big g ambazo hazina sukari yani Sugar-free chewing gums ambazo ni nzuri kwa meno na kinywa cha binadamu. Kwa sasa utaratibu uliopo ukikutwa unatema big g chini au unatafuna ovyo unapigwa faini.

5. Majina ya watoto

Ujerumani na Denmark kisheria hawaruhusiwi kuwapa watoto majina yoyote nje ya majina 7000 ambayo tayari yamepitishwa, ikitokea mtu atapenda kumuita mwanae jina alipendalo basi atatakiwa kuomba kibali maalum kanisani alafu baadae maombi hayo yanawasilishwa Serikalini, jina likipitishwa basi unaruhusiwa kulitumia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni