MFUNGWA
ambaye wapiganaji wa kundi la ISIS lilimtuhumu kuwa jasusi wa Israel
(Mossad) hivi majuzi aliuawa kwa kupigwa risasi kichwani katika jangwa
la Sinai, Misri.
Kwa
mujibu wa video zilizopatikana, mfungwa huyo anaonekana akiwa amesimama
katika shimo akichimba kaburi lake, akapigwa risasi nyuma ya kichwa na
kusukumiziwa katika kaburi hilo.
ISIS wamesema mtu huyo alikuwa anafanya ujasusi na kuripoti kwa serikali ya Israel kuhusu shughuli za ISIS eneo hilo la Misri.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni