Jumamosi, 13 Juni 2015

BIBI HILARY CLINTON AHUTUBIA NEW YORK

 
Bi Clinton ahutubia umma New York
Mgombea wa kiti cha urais nchini Marekani bi Hillary Clinton amefanya mkutano wake wa kwanza wa hadhara tangu atangaze nia ya kuwania kiti cha Urais.
Bi Clinton ambaye anapigiwa upatu wa kutwaa tikiti ya chama cha Democratic katika uchaguzi huo wa urais, ametangaza ruwaza yake mbele ya maelfu ya mashabiki wake mjini New York.
Wandani wa kampeini yake wanaazimia kuimarisha ushindani wake machoni mwa wapiga kura watakaomchagua atakayerithi kiti cha rais Obama.
Kulingana na kura ya maoni ushawishi wake umekuwa ukidorora tangu atangaze niya yake mwezi Aprili.

Bi Clinton alikuwa ameandamana na mumewe aliyekuwa rais wakati mmoja Bill Clinton na mwanaye wa kike Chelsea.

 
Bi Clinton aliandamana na mumewe Bill na mwanawe Chelsea
Bi Clinton 67 alitoa video Ijumaa hii akinadi sera zake kuwa zinalenga kutetea maslahi ya ''raia wa kawaida tu Mmarekani.''
''Kila mmoja wetu anahaki ya kupata maisha mazuri tu na kuishi kwa amani na ustawi kadri ya uwezo wake aliopewa na Mwenyezi Mungu''
''Hiyo ndiyo ndoto yangu hiyo ndiyo vita tunayopaswa kupigania ''alisema bi Clinton.
''Babangu mimi alikuwa mtoto wa mfanyikazi wa kawaida kiwandani aliyejikakamua na kuanzisha biashara ndogo''

Clinton anapigiwa upatu kutwaa tikiti ya chama cha Democratic
Mamangu pia japo hakuenda chuoni alinisomesha nikahitimu chuoni''
''Kila Mmoja wetu anahitaji kuwa na ndoto na mtu anayemuiga ambaye ameanzia chini maisha yake na kuimarika kufikia ufanisi wa kutajika ,alisema bi Clinton
Huu unatizamwa kama mwamko mpya katika kampeni ya bi Clinton.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni