Ijumaa, 26 Juni 2015

AOA SIKU 3 KABLA YA KUAGA DUNIA

Alioa siku 3 tu kabla ya kuaga dunia
Kijana mmoja barubaru alimuoa mpenzi wake siku tatu tu kabla yake kuaga dunia kutokana na Saratani ya damu lukaemia.
Omar Al Shaikh alimuoa mpenzi wake Amie Cresswell, wote wenye umri wa miaka 16, katika wadi ya hospitali kuu ya Malkia Elizabeth ilioko Birmingham Uingereza.
Omar, aliaga dunia Jumatatu hii siku tatu tu baada ya kufunga pingu za maisha na Amie.
Omar aliaga dunia baada ya kukosa mtu ambaye damu yake inayoingiana na yake.
Omar alimchumbia Amie baada ya kufahamishwa na madaktari kuwa alikuwa na siku 5 tu za kuishi.
Mamake bi Mirabela anasema kuwa alijizatiti hadi siku yake ya mwisho.
''amejikaza sana na kupanga kila kitu alichotaka kifanyike''alisema mamake

 
null
Omar (wa kwanza kulia) aliaga dunia baada ya kukosa mtu ambaye damu yake inayoingiana na yake
"alitaka sana kumuoa Amie,alikuwa akinieleza kuwa angefurahia sana akisimama mbele ya haki na kumweleza mwenyezi mungu kuwa Amie alikuwa ni mkewe''
Shangazi yake Anca Dumitriu alisema "Ilikuwa ni siku nzuri sana kwani wote walifurahia sana''
Omar alimwambia Amie ''Wewe ni mke wangu sasa''
Mwanajeshi huyo mtarajiwa Omar, aligunduliwa kuwa anaugua Lukemia baada ya kuanguka na kuzirai alipokuwa akicheza mpira.
Kutokana na asili yake ya Kirumi na Kiarabu ilikuwa vigumu sana kupata mtu mwenye chembechembe zitakazoingiana.
Mamake alisema tangu afahamishwe kuhusu kuzoroteka kwa hali yake ya siha mapema mwezi huu Omar amejitahidi kuwa mchangamfu hadi alipoaga dunia.
''Aliaga dunia usingizini''

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni