Ijumaa, 26 Juni 2015

MWANAMKE NA MTOTO WAKE WAPATIKANA WAKIWA HAI KUFUATIA AJALI YA NDEGE

Mwanamke mwenye umri mdogo pamoja na mtoto wake wamekutwa wakiwa hai siku tano baada ya ndege waliokuwemo kuanguka kwenye msitu magharibi mwa Colombia.
Mwanamke huyo Maria Nelly Murillo, 18, na mtoto wake wa mwaka mmoja wamekutwa na waokoaji karibu na ndege hiyo yao ndogo aina ya Cessna iliyoanguka kwenye Mkoa wa Choco.
 Mkuu wa Kikosi cha Anga cha Kolombia ameelezea kuwa kunusurika kwa mama huyo na mtoto wake ni muujiza. Murillo alikuwa na majeruhi na kuungua lakini mtoto wake alikuwa mzima kabisa.
     Mtoto wa mwanamke huyo akiwa amebebwa na muokoaji

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni