Jumanne, 30 Juni 2015

CHILE HIYOO FAINALI KOPA AMERICA

Mashabiki wa timu ya Chile
Mashabiki wa Chile kusubiri Fainali baada ya timu yao kushinda Peru kwenye nusu Fainali
Wenyeji wa kombe la Copa America Chile wamefuzu kufika fainali mara ya kwanza kwa miaka 28. Hii ni baada ya kuwanyuka Peru mabao mawili kwa moja katika mchuano uliofanyika mjini Santiago.

Nusura kiungo wa kati wa Chile Arturo Vidal kuondolewa mapema, hata hivyo bahati mbaya ilikuwa kwa mlinda lango wa Peru Carlos Zambrano aliyepewa kadi nyekundu.
Aliyekuwa mshambuliaji wa klabu wa QPR ya Uingereza Eduardo Vargas alisaidia Chile kupata bao la kwanza dakika ya 42.
 
null
Eduardo Vargas alisaidia timu yake kupata magoli mawili
Hata hivyo Peru ilisawazisha pale Gary Medel alipojifunga bao. Vargas ndiye aliipatia Chile bao la pili na la ushindi katika dakika ya 64.
Chile haijawahi kushinda kombe la Copa kwa karibu karne moja. Chile wanaingia fainali hapo Jumamosi ambapo huenda wakachuana na Argentina au Paraguay.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni