Sehemu iliyokuwa imeandaliwa kwa ajili ya kutangaza nia ya kugombea urais katika Ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency.
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Frederick Sumaye akitangaza nia ya kugombea urais mbele ya wananchi waliohudhuria mkutano huo leo.
Meza
kuu, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Ester Sumaye (kushoto) Waziri Mkuu
Mstaafu, Frederick Sumaye (katika) Mwenyekiti wa UVCCM wa Kinondoni,
Shabani Uronu, pamoja na Katibu Mwenezi CCM, Kata ya Kiluvya, Juma
Semindu.
WAZIRI
Mkuu Mstaafu Mhe. Frederick Tluway Sumaye leo ametangaza nia ya kugombea
urais wa Tanzania kwa mwaka wa 2015 kupitia tiketi ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM).
Akizungumza
leo mbele ya wananchi na wanahabari katika Ukumbi wa Hoteli ya Hyatt
Regency (zamani Kilimanjaro Hoteli) jijini Dar es Salaam, Sumaye amesema
kuwa ameamua kutangaza nia ya kuwa mgombea urais kutokana na alivyoweza
kujipima mwenyewe, kujishauri na kutafuta ushauri kutoka kwa watu
wengine na kuona kweli anafaa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Alisema
kuwa amejitathimini na kuona kuwa yeye ndiye anayetosheleza kuwa
kiongozi wa nchi hii kutokana na jinsi alivyoweza kuongoza nchi hii
akiwa Waziri Mkuu kwa zaidi ya miaka 9 na hivyo anastahili kuiongoza
nchi.
Aliongeza
kuwa amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi katika utumishi wa
umma, kama ubunge, unaibu waziri, Uwaziri na hatimaye kuwa Waziri Mkuu
wa Tanzania.
“Katika
uongozi wangua nilijitahidi sana kusimamia uchumi wa taifa kama vile,
kusimamia uchumi, kuvunja Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam iliyokuwa
ikiongoza kwa uchafu wa mazingira miaka ya 1996, kutengeneza madawati
kwa shule zote za msingi, kuweka televisheni ya taifa, mpango wa
maendeleo Elimu (MMEM) na mambo mengine, ”alisema.
Vilevile
alieleza juu ya kufanya kazi kwa muda huo wote katika ngazi mbalimbali
kuwa ni dhahiri nchi anaifahamu pamoja na shida za wananchi pamoja na
matatizo yao anayajua, kila eneo na kila kanda hivyo akiteuliwa kuwa
rais hatahitaji kujifunza juu ya nchi ya Tanzania.
Wakati
akizidi kufafanua alieleza malengo yake endapo akiteuliwa kuwa rais kuwa
lazima atazingatia mambo yafuatayo ili kuweka uchumi imara katika nchi
yetu ya Tanzania ikiwa ni pamoja na kulinda muungano pamoja na amani na
utulivu, kuimarisha uchumi, kupambana na maovu ya rushwa kama vile
ufisadi na madawa ya kulevya na mauaji, kuboresha huduma za jamii na
ajira pamoja na michezo.
Waziri
Mkuu Mstaafu alipoulizwa swali juu ya ambao wote tayari wamekwisha
tangaza nia ya kugombea urais kwa mwaka 2015 kuwa nani anamwona kuwa
kinara zaidi yake alisema kuwa yeye ndiye anafaa kuwa kiongozi wa nchii
hii kwani wote waliokwisha tangaza haoni kama wana imani na kuongoza
nchi yetu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni