Jumatatu, 29 Juni 2015

HABARI ZA MBABAZI KUREJEA KAMPALA LEO ZAZUA TAFRANI

Hii ndiyo itakayokuwa mtihani mkubwa zaidi kuwahi kumkabili rais Museveni ndani ya chama cha NRM.
Taharuki imetanda mjini Kampala Uganda baada ya habari kuenea kuwa mpinzani mkuu wa rais Yoweri Museveni ,aliyekuwa waziri mkuu Amama Mbabazi anarejea leo.
Mwandishi wa BBC aliyeko huko anasema kuwa polisi wametumwa katika barabara ya kutoka Kampala hadi kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe.
Bwana Mbabazi anasemekana kuwa anarejea kutoka kwa ziara ya kimataifa iliyompeleka Uingereza na Marekani.

Wafuasi wake wamepanga kumkaribisha kwa shangwe na vigelegele.
Yamkini wamepanga kuwa na msafara wa magari yaliyojaa wafuasi wake kumkaribisha.
Amama Mbabazi alitangaza majuma mawili nia ya kushindana na rais Muuseveni kuwania uwenyekiti wa chama cha National Resistance Movement na hatimaye kuwania kiti cha urais.
Wawili hao walikuwa washirika wa karibu kwa zaidi ya miaka 40 .
 
null
Picha ya Amama Mbabazi
Rais Museveni ametawala Uganda tangu mwaka wa 1986 na anatarajiwa kuwania urais kwa muhula wake wa nne.
Museveni alimfuta kazi bwana Mbabazi mwaka uliopita katika hatua iliyotafsiriwa na wachanganuzi wa kisiasa nchini humo kuwa mbinu ya kukandamiza mpinzani wake mkuu.
Bwana Mbabazi anakabiliwa na changamoto kubwa ya kushinda uteuzi katika chama tawala cha National Resistance Movement (NRM).
Rais Museveni tayari ameidhinishwa na kamati kuu ya chama japo anahitaji kupokea ithibati ya wanachama katika mkutano mkuu wa wajumbe.
Iwapo atakonga nyoyo za wajumbe wa NRM sasa Mbabazi sasa atawania urais dhifi ya Museveni
Mwandishi wa BBC Rachael Akidi anasema kuwa hii ndiyo itakayokuwa mtihani mkubwa zaidi kuwahi kumkabili rais Museveni ndani ya chama cha NRM.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni