Jumatatu, 29 Juni 2015

MFUNGWA ATOROKA GEREZANI NEW YORK AKAMATWA

David Sweat aliyekamatwa baada ya kutoroka gerezani katika jimbo la New York alikokuwa akitumikia adhabu ya kifungo kutokana na makosa ya mauaji
Polisi nchini Marekani wamempiga risasi na kumkamata mfungwa aliyetoroka gerezani katika jimbo la New York alikokuwa amefungwa kutumikia adhabu kutokana na makosa ya mauaji wiki tatu zilizopita.
David Sweat alikamatwa karibu na mpaka wa Canada baada ya afisa wa polisi kumng'amua akifanya mazoezi ya kukimbia kando ya barabara.
Mfungwa mwenzake aliyetoroka Richard Matt aliuawa na polisi Ijumaa. Watu hao wawili walitumia zana imara kuweza kutoroka kutoka gereza lenye ulinzi mkali la Clinton na kusababisha msako mkubwa wa polisi kufanyika.
Gavana wa jimbo la New York, Andrew Cuomo, amesema jinamizi la wahalifu hao limekwisha.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni