Kiongozi wa Zimbabwe na mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Robert Mugabe
ameikosoa vikali mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za uhalifu
ya ICC .
Baada ya rais wa Sudan kulikwepa agizo la mahakama hiyo iliyoamuru
akamatwe,wakati akihudhuria mkutano wa viongozi wa bara la Afrika
uliomalizika jana nchini Afrika Kusini: Rais huyo wa Sudan hatimaye
aliondoka na kurudi nyumbani.
Shirika la Habari la Afrika, lenye makao yake nchini Afrika Kusini, lilimnukuu Mugabe akisema wakati wa kufunga mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika mjini Johannesburg jana usiku kwamba Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu haitakiwi barani Afrika.
Mugabe alisema,"hapa si makao makuu ya ICC. Hatuitaki katika kanda hii kabisa." Mugabe ambaye ni Mwenyekiti wa mwaka huu wa Umoja wa Afrika, wadhifa unaozunguka miongoni mwa viongozi wa Umoja huo alisema mkataba uliounda ICC haukutiwa saini na Umoja wa Afrika bali nchi moja moja, akiongeza kuwa kuna fikra ya kujitoa katika mahakama hiyo.
Afrika Kusini imesaini waraka unaounda mahakama hiyo ya kimataifa, lakini baadhi ya viongozi wa Afrika wanasema mahakama hiyo inawaandama tu viongozi wake wa kiafrika na Umoja wa Afrika umesema wajumbe katika mkutano huo wa kilele wa Johannesburg wana kinga ya kibalozi.
Shirika la habari la Africa lilioripoti kwamba, kwa mujibu wa Rais Mugabe, Rais jacob Zuma wa Afrika kusini alisema hatoiruhusu polisi kumkamata Rais Bashir. Msema wa ofisi ya Zuma alitaka maswali yote aulizwe msemaji wa serikali bibi Phumla Williams ambaye hakuweza kupatika hii leo kwa kuwa ni siku ya mapumziko ya kitaifa nchini humo.
Mjini The Hague, naibu mwendesha mashtaka wa mahakama hiyo ya uhalifu ya kimataifa James Stewart alisema Afrika Kusini ilikuwa na jukumu kisheria kumkamata Rais Bashir ili afikishwe mahakamani mbele ya mahakama hiyo.
Kiongozi wa Sudan aliyewasili Khartoum anasakwa na mahakama hiyo ya ICC kujibu mashtaka ya kuhusika na uhalifu wa kivita, unaohusishwa na mgogoro wa jimbo la magharibi mwa Sudan la Darfur.
Mwanasheria Nickl Kaufman anayewawakilisha wahanga kadhaa katika kesi ya Darfur kwenye mahakama ya ICC, leo aliwasiliana na mwendesha mashtaka wa mahakama hiyo, akiwataka majaji kuwasilisha hati rasmi ya malalamiko kwa serikali ya Afrika Kusini kutokana na kushindwa kutii amri ya mahakama hiyo na kumkamata Bashir na kutaka pia suala hilo liwasilishwe mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Wakati huo huo, Marekani imeelezea kusikitishwa kwake kutokana na rais Bashir kuhudhuria mkutano huo wa viongozi wa Umoja wa Afrika na kushindwa kwa Afrika Kusini kumtia nguvuni. Marekani yenyewe si mwanachama wa ICC, kwa kuwa imekataa kusaini waraka uliounda mahakama hiyo.
Mwandishi: Salma Mkalibala,AP
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni