Jumanne, 16 Juni 2015

KIONGOZI WA ALQAEDA YEMEN AUAWA

 
Kiongozi wa Al Qaeda nchini Yemen 
 
Tawi la kundi la Al Qaeda nchini Yemen limethibitisha kuuawa kwa kiongozi wake wakati wa shambulizi la ndege isiyokuwa na rubani ya Marekani.

Ripoti kutoka kwa maafisa wa usalama nchini Yemen zinasema kuwa Nasser al-Wuhayshi aliuawa siku ya ijumaa katika mji wa bandari wa Mukala.

Kundi lake limelaumiwa kwa kupanga mashambulizi kadhaa dhidi ya Marekani likiwemo jaribio la kuilipua ndege ya Marekani mwaka 2009, pamoja na shambulizi katika gazeti la Charlie Hebdo mji Paris nchini Ufaransa mwezi Januari mwaka huu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni