Ijumaa, 5 Juni 2015

MBEKI ALITOA FEDHA KWA FIFA - WAZIRI

Thabo Mbeki
Waziri wa michezo wa Afrika Kusini, Fikile Mbalula, sasa anasema rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki ndie aliyeruhusu ulipwaji wa fedha, dola milioni 10 kwa FIFA, hela ambayo sasa inakumbwa na madai kwamba ilikuwa rushwa .
Utawala wa Afrika Kusini umekuwa ukisisitiza kwamba ulikuwa ni mchango wa kusaidia kukuza soka katika nchi za Caribbean.

Lakini waendesha mashtaka wa Marekani wanadai ilikuwa hongo, iliyoshawishi kupewa uenyeji wa kombe la dunia mwaka 2010 .

Bwana Mbeki mwenyewe hajatoa kauli yoyote kuhusiana na swala hilo.

Barua inayosemekana iliandikwa na shirikisho la soka nchini Afrika Kusini, inaonekana kuongeza uzito kwenye shutuma kwamba serikali ya nchi hiyo ilitoa malipo hayo kwa siri

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni