Taarifa
kutoka wizara ya sheria nchini Iraq imetangaza kifo cha Tariq Aziz
aliyekuwa mshauri wa karibu wa aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Saddam
Hussein.
Tariq Aziz amefariki dunia mapema leo akiwa angali jela
alikokuwa akizuiliwa tangu alipokamatwa wakati nchi hiyo ilipovamiwa
kivita na Marekani iliyoungo'a utawala wa Saddam Hussein.Tariq Aziz alikuwa ni mkristo pekee katika serikali ya Sadam Hussein na amefariki akiwa umri wa miaka 79.
Alihudumu kama naibu waziri na pia waziri wa mambo ya nje wa serikali hiyo ya Sadam Hussein .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni