Afisa
wa ngazi ya juu katika kitengo kinachohusiana na haki za kibinadamu
kwenye shirika la umoja wa mataifa ametoa wito kwa rais mpya wa Nigeria
Muhammadu Buhari kufanya hima ili kuanzisha uchunguzi kuhusu madai ya
ukiukaji wa haki za kibinadamu unaosemekana ulifanywa na vikosi vya
kijeshi vinapokuwa vikipambana na kundi la Boko Haram.
Shirika la
kutetea haki za kibinadamu Amnesty International (AI) linadai kuwa zaidi ya
watu elfu 8 walifariki wakiwa katika vizuizi vya maafisa salama.Afisa huyo wa umoja wa mataifa, Zeid Ra'ad Al-Hussein, ameshtumu ukatili unaofanywa na kundi hilo la Boko Haram dhidi ya raia wasio na hatia.
Serikali ya Nigerian imesema zaidi ya watu 30 wameuawa katika shambulio la hapo jana linaloshukiwa limefanywa na wapiganaji hao wa Boko Haram ambao wamehusika katika mashambulio mengine mengi yaliyosababisha maafa kama hayo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni