Jumatano, 24 Juni 2015

MLIPUKO WAUA 12 MOGADISHU

Mogadishu Somalia
Mlipuaji wa kujitolea muhanga ameligongesha gari lake na lile la kijeshi katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu na kusababisha mlipuko mkubwa.

Ripoti zinasema kwamba takriban watu 12 waliuawa na wengine kujeruhiwa wengi wakiwa raia.

Shambulizi hilo lilitokea karibu na ubalozi wa falme za kiarabu UAE

Vyombo vya habari nchini Somalia vimeripoti kwamba balozi amenusurika mlipuko huo ambao umeutaja kama jaribio la mauaji.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni