Ripoti
za vyombo vya habari nchini Marekani zinasema kuwa watu 18 wameaga
dunia katika eneo la Uchina la Xinjiang katika makabiliano na polisi
katika eneo la ukaguzi.
Radio Free Asia inasema kuwa watu hao wa kabila la Uighurs walitumia visu na mabomu kuwashambulia maafisa wa polisi.Hakujakuwa na mawasiliano rasmi kuhusu tukio hilo lakini wafanyakazi wa hospitali katika mji wa Kashgar wameiambia BBC kuwa maafisa hao wa polisi walipokea matibabu.
Moja ya lengo huenda ni kuweka vikwazo vikali kwa waislamu wa Uighurs katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadan.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni