Wakati
Shirikisho la soka Duniani, FIFA likitangaza leo kwamba Februari 26
mwakani ndio siku ya uchaguzi mkuu wa Rais, limetokea tukio la aina yake
katika mkutano wa Sepp Blatter na Waandishi wa habari.
Sepp Blatter ambaye alitangaza kujiuzulu wadhifa wa Urais wa FIFA ametupiwa pesa na mtu aliyevamia mkutano wake.
Mvamizi
huyo aliyetambuliwa kwa jina la Lee Nelson, raia wa Uingereza
aliondolewa ukumbini humo mara moja na maafisa wa usalama wa FIFA.
Nelson (kushoto) kabla ya kufanya tukio hilo
Blatter aliyekuwa ameudhika sana na tukio hilo kabla ya kuondoka ukumbini alisema ‘halikuhusiana kwa njia yeyote na soka’ .
Blatter alitangaza mabadiliko kadha ikianza na tarehe ya uchaguzi.
Aidha
Viongozi watakaokuwa na nia ya kurithi kiti hicho cha rais wa FIFA,
sharti wawasilishe rasmi maombi yao kabla ya tarehe 26 mwezi Oktoba
mwaka huu.
Rais
wa shirikisho la soka barani Ulaya (Uefa) Michel Platini, anadaiwa
kupata shinikizo kutoka kwa viongozi wengi wa bara hilo kuwasilisha ombi
lake la kuwa rais wa FIFA.
Mkutano
huo wa leo pia ulitaja baadhi ya mambo yatakayorekebishwa ikiwa ni
pamoja na kuweka kikomo cha muhula cha urais na viongozi wengine wa
ngazi ya juu wa shirikisho hilo.
Hatua ya kuchapisha mishahara na marupurupu ya viongozi wa ngazi ya juu wa shirikisho hilo pia ilijadiliwa.
Aidha FIFA itateua jopo la watu 11 watakaoanza uchunguzi wa kina kubaini njia za kukabiliana na rushwa na ubadhirifu.
Jopo hilo maalum ndilo litakaloendesha mabadiliko katika Fifa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni