Ajali mbaya imetokea leo jijini Mbeya baada ya magari matatu kugongana katika eneo la Mama John ambapo magari yaliyohusika katika ajali hiyo ni basi la Al Saedy linalofanya safari zake kutoka Mbeya kwenda mkoani Dar es Salaam, Noah na gari lingine dogo (IT).
Ajali hiyo imetokea leo asubuhi wakati dereva ambaye hajafahamika jina mara moja wa basi la Al Saedy lenye namba za usajili T T830 BQG lililokuwa limetokea kituo kikuu cha mabasi jijini Mbeya kuelekea Dar es Salaam alipokuwa akitaka kulipita gari dogo katika eneo hilo.
Wakati anajaribu kulipita gari hilo ndipo akakutana uso kwa uso na gari dogo aina ya Noah lenye namba za usajili T 969 BWG lililokuwa likitokea Uyole na likiwa na watu watano walionusurika kifo.
Taarifa za mashuhuda kutoka eneo la tukio zinasema kuwa baada ya Basi hilo la abiria kugongana na Noah gari lingine dogo IT lililokuwa likielekea Tunduma kutoka Dar es Salaam liligonga Noah upande wa nyuma.
Kutokana na kilichoshuhudiwa katika eneo la ajali, mashuhuda wametanabaisha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi na kutokuwa makini kwa dereva wa basi hilo ambalo abiria wake wote wamenusurika kujeruhiwa.
Aidha ajali hiyo imesababisha majeraha makubwa kwa dereva wa Noah ambaye amevunjika mguu wake pamoja na dereva wa gari dogo IT ambao wote waliwahishwa hospitalini kupatiwa huduma ya kwanza (wote hawakufahamika majina yao mara moja). Hakuna vifo katika ajali hiyo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni