Alhamisi, 30 Julai 2015

KENYA YAUA AL SHAABAB 3

Wapiganaji wa Al Shabab
Jeshi ya Kenya linasema limewaua magaidi watatu wa Al Shabab katika eneo la Lamu lililoko Pwani ya Kenya.
Wanajeshi watano walijeruhiwa katika shambulio hilo ,wakati gari la wanajeshi lilipogongwa kilipuzi na kulipuka.
Msemaji wa jeshi la Kenya, Kanali David Obonyo amesema gari hilo la jeshi lilikuwa linafanya doria ya kawaida na ndipo likakanyaga kilipuzi kilichotegwa. Hivyo wanajeshi hao walianza mashambuzi na kufanikiwa kuwaua magaidi watatu na kuzipata bunduki mbili pamoja na risasi kumi na saba.
Eneo la Lamu limekumbwa na msururu wa mashambulizi kwa muda sasa. Mwezi Juni wapiganaji kumi na mmoja, akiwemo raia wa Uingereza, na wanajeshi wawili waliuawa , baada ya Al Shaabab kuvamia kambi ya jeshi eneo la Lamu.
Mwaka jana watu wasiopungua 60 waliuawa na AL Shababa katika shambulio eneo la Mpeketoni Lamu, siku mbili mfululizo. Na siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa za magari ya abiria kuvamiwa na wanamgambo hao kwenye barabara ya Lamu, ingawa Polisi wamekanusha habari hiyo.
Hata hivyo msako Mkubwa unaendelea katika msitu wa Boni wanakodaiwa kujificha magaidi hao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni