Jumatano, 19 Agosti 2015

MAN U YATAKATA KWA BRUGGE

Marouane Fellaini aliipa bao la ushindi Manchester United
Manchester United imeanza vizuri mchezo wa kwanza wa mchujo kuwania nafasi kuingia hatua ya makundi ya michunao ya klabu bingwa barani ulaya baada ya kupata ushindi wa 3-1 dhidi ya Club Brugge ya Ubelgiji. 

Brugge ilipata bao lao mapema dakika ya 8 ya mchezo baada ya kiungo wa Man U Michael Carrick kujifunga.

Mshambuliaji mpya wa kikosi hicho cha mashetani wekundu Memphis Depay akasawazisha bao hilo dakika ya 14 kabla ya kuongeza bao la pili dakika 43, kiungo aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Wayne Rooney, Mbelgiji Marouane Fellaini, akifunga bao la tatu lilihitimisha ushindi huo.

Matokeo mengine ya michezo ya mchujo kuwania kuingia hatua ya makundi ya klabu bingwa ulaya ni:
Astana 1 APOEL Nicosia 0
BATE Borisov 1 Partizan Belgrade 0
Lazio 1 Bayer Leverkusen 0
Sporting CP 2 CSKA Moscow 1

ALBINO WATANO WAREJESHEWA VIUNGO USA

Albino 5 raia wa Tanzania waliokatwa viungo wamerejeshewa viungo bandia Marekani
Watoto watano wa Tanzania wenye ulemavu wa ngozi waliokuwa wamekatwa viungo vya miili yao wamewekewa mikono na miguu ya bandia katika hospitali iliyopo nchini Marekani.
Watoto hawa ni miongoni mwa mamia ya watu wanye ulemavu wa ngozi nchini humo ambao wamekuwa wakiwindwa na watu wanaotaka viungo vya miili yao kwa shughuli za kishirikina
Watoto hao, mmoja wa kike na wanne wa kiume kutoka mikoa ya Kaskazini Magharibi na Kusini Magharibi mwa Tanzania, wamekuwa wakipokea matibabu hayo katika hospitali ya watoto Philadelphia Shriners Hospital iliyopo jijini New York.

UKAWA WAKITANGAZA MAJIMBO WALIYOGAWANA KATIKA UCHAGUZI MKUU

 Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi,  Nderakindo Kessy (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya chama hicho, Ilala Dar es Salaam jana, wakati akitangaza majimbo yaliyochini ya vyama vinavyounda Ukawa ambayo vyama hivyo vitasimamisha wagombea wao katika uchaguzi mkuu. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha NLD, Masudi Makunjunga.
 Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Shaweji Mketo (wa pili kulia), akizungumza katika mkutano huo na waandishi wa habari. Kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha NLD, Masudi Makunjunga, Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi,  Nderakindo Kessy na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika.
 Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika, akizungumza katika mkutano huo.

Jumatano, 12 Agosti 2015

RAIS WA ZAMANI WA MAREKANI JIMMY CARTER ASEMA ANA SARATANI


Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter ametangaza kuwa ana maradhi ya saratani. 

Carter mwenye umri wa miaka tisini, na siku za hivi karibuni alifanyiwa upasuaji wa ini.

Jimmy amesema kuwa imebainika kuwa ana saratani ambayo imekwisha sambaa katika baadhi ya sehemu za mwili wake.

Ameongeza kuwa yupo katika mpango wa kuweka vizuri ratiba yake kwa lengo la kupata matibabu zaidi.

Jimmy Carter toka aondoke madarakani ,amekua akijisughulisha na kazi za kuhudumia jamii duniani kote

Jumamosi, 8 Agosti 2015

RAIS KIKWETE AZINDUA BENKI YA MAENDELEO YA KILIMO TANZANIA (TADB) DAR ES SALAAM

 Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akihutubia wakati akizindua Benki ya Maendeleo ya Kilimo Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam leo asubuhi. Kulia ni Waziri wa Fedha, Saada Salum Mkuya na Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Stephen Wasira. Rais Kikwete alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa benki hiyo. 
 
Uzinduzi wa awamu ya pili wa benki hiyo utafanyika kwenye maonyesho ya Nanenane kitaifa mkoani Lindi.

Jumamosi, 1 Agosti 2015

CHAD YADAI KUUA BOKO HARAM 100

Chad 'imewaua wapiganaji 100' wa Boko Haram
Jeshi la Chad linasema kuwa limewaua zaidi ya wanamgambo 100 wa Boko Haram katika kipindi cha majuma mawili yaliyopita.
Wanamgambo hao wanasemekana waliuawa katika mapigano makali katika visiwa vilivyoko kwenye ziwa Chad.
Aidha taarifa hizo bado hazijathibitishwa.