Rais
alitoa agizo hilo baada ya kikao baina yake na makatibu wa wizara
kilichofanyika Ikulu siku chache baada ya kuapishwa, akisema ofisi yake
ndiyo itakayotoa kibali kwa watumishi ambao wana safari za nje.
Kwa mujibu wa waraka huo, sharti la kwanza linalotakiwa kuzingatiwa na watumishi hao ni kuomba kibali kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
Pili, kwa
mujibu wa mwongozo huo, maombi yawasilishwe kwa msajili wa hazina kabla
ya kwenda kwa Katibu Mkuu Kiongozi ili aweze kujenga hoja kwa kuzingatia umuhimu wake
na tija itakayopatikana kutokana na safari hiyo.
Tatu,
mtendaji mkuu wa shirika au taasisi apime maombi ya safari husika ili
kuona kama yana tija na yana umuhimu wa kuombewa kibali kwa Katibu Mkuu Kongozi, kabla ya kuwasilishwa kwa msajili wa hazina, kwa mujibu wa
mwongozo huo.