Jumanne, 10 Novemba 2015

MAPIGANO YA JOGOO YAUA WATU 10

 
Vita vya jogoo vyasababisha vifo vya watu 10

Takriban watu 10 wamepigwa risasi na kuawa baada ya makundi mawili kutofautiana kuhusu jogoo yupi aliyeibuka mshindi katika vita katika jimbo la Guerrero Mexico.

Miongoni mwa wale waliouawa ni ni mvulana mwenye umri wa miaka 12 aliyepigwa risasi katika mji wa Cuajinicuilapa.

Watu wengine 7 walijeruhiwa vibaya.

Uchunguzi wa awali uliashria kuwa mashabiki wa jogoo hizo mbili walitofautiana kuhusu ni yupi aliyeibuka mshindi.

Hata hivyo duru zinasema kuwa huenda ukumbi huo wa mapigano ya majimbi ulivamiwa na watu walikuwa wamejihami kwa bunduki.

Hadi kufikia sasa,haijulikani iwapo magenge yanayoshamiri mjini Guerrero ndiyo yaliyotekeleza mauaji hayo ya kinyama.

Mwaka uliopita wanafunzi 43 walitoweka katika mji wa Iguala na kuweka tatizo la magenge katika majimbo ya Mexico katika rubaa za kimataifa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni