Jumanne, 9 Februari 2016

MAPIGANO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI YAZUKA TENA WILAYANI MVOMERO, MBUZI ZAIDI YA 70 ZAKATWA KATWA MAPANGA

Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvui Mh.Mwigulu Nchemba sambamba na Mbunge wa jimbo la Mvomero Mh Sadick Murad (mwenye shati ya drafti),ikiwemo na Kamati ya Ulinzi na Usalama sambamba na wananchi wakishuhudia tukio la mgogoro wa Wakulima na Wafugaji,ambapo takribani mbuzi zaidi ya 70 wamekatwa katwa mapanga na watu wasiojulikana,ambapo Waziri huyo ameahidi sheria na hatua za kudumu za tatizo hilo kuchukuliwa haraka iwezekanavyo.
 Baadhi ya Mbuzi waliokatwa katwa na mapanga .
 Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh. Mwigulu Nchemba akiongozwa na wafugaji kabila la Wamasai kufuatia mgogoro wao na Wakulima na kupelekea uharibifu mkubwa wa kuuawa kwa  mbuzi zaidi ya 70. 
 
 Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mh. Mwigulu Nchemba sambamba na Mbunge wa jimbo la Mvomero Mh Sadick Murad (mwenye shati la drafti), ikiwemo Kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya ya Mvomero na wananchi mbalimbali wakishuhudia tukio la kuuawa kwa mbuzi zaidi ya 70 wakiwa wamekatwa katwa mapanga na watu wasiojulikana, ambapo Waziri huyo ameahidi sheria na hatua za kudumu za kumaliza tatizo hilo kuchukuliwa haraka iwezekanavyo.
 Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mh. Mwigulu Nchemba akiwahutubia Wananchi wa Wilaya ya Mvomero katika kijiji cha Dihinda mkoani Morogoro kufuatia mgogoro mkubwa kuzuka kati ya Wakulima na wafugaji, ambapo inaelezwa kuwa katika tukio hilo mbuzi  na kandoo zaidi ya 70 wakiwa wamekatwa katwa mapanga na watu wasiojulikana.Waziri Mwigulu Nchema ameahidi  kuwa sheria na hatua za kudumu za tatizo hilo kuchukuliwa haraka iwezekanavyo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni