Jumanne, 8 Machi 2016

Watu saba wauawa kwa kuchomwa moto Malawi

Polisi nchini Malawi wanasema genge moja la watu limewauwa watu saba kwa kuwachoma moto kwa madai ya kukutwa na mifupa ya binaadamu kwa ajili ya matumizi ya kichawi kusini mwa nchi hiyo.
Mkuu wa polisi wa wilaya ya Nsanje, Kirdy Kaunga, anasema watu hao walikutikana na mifupa ya binadaamu na genge hilo likajiamulia kuchukua hatua mikononi mwao kwa kuwawasha moto wakitumia petroli.
Maafisa wanasema bado wanaendelea na uchunguzi iwapo mifupa hiyo ilikuwa ni ya watu wenye ulemavu wa ngozi, yaani albino.
Katika nchi kadhaa za Kiafrika, zikiwamo Malawi, Msumbiji na Tanzania, watu wenye ulemavu wa ngozi huandamwa kwa mashambulizi yanayolenga kukatwa viungo vyao ambavyo hutumiwa kwenye mambo ya kishirikina.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni