Jumatatu, 30 Mei 2016

SHEKHE AUAWA KATIKA FUMANIZI

JESHI la Polisi Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma, linamshikilia mkazi wa Kijiji cha Likweso, Tarafa ya Mchoteka, Ally Mchumwa
kwa tuhuma za mauaji ya Shekhe wa kijiji hicho.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Zubery Mwombeji, alisema tukio hilo limetokea Mei 22, mwaka huu, baada ya mtuhumiwa (Mchumwa), kumfumania akifanya tendo la ndoa na mkewe.

"Mauaji haya yametokea saa tatu asubuhi wakati marehemu ambaye amefahamika kwa jina la Seleman Mwalabu (45), mtuhumiwa na mkewe Mariamu Husein, wakisaidiana kuvuna njugu shambani.

"Wakati wakiendelea na kazi hiyo, mtuhumiwa alitoka kidogo na kumuacha marehemu pamoja na mkewe wakiendelea na kazi hiyo, aliporejea hakuwakuta shambani hivyo akashtuka," alisema.

Kamanda Mwombeji alisema wakati mtuhumiwa akiwa katika kwenye sintofahamu hiyo, alisikia sauti ikitoka porini jirani na shamba lake hivyo aliamua kwenda na kumkuta mkewe na mtuhumiwa wakiwa uchi wa mnyama ikiashiria wametoka kufanya tendo la ndoa.

Kutokana na hali hiyo, mtuhumiwa alichomoa kisu na kumchoma nacho marehemu shingoni, kufariki papo hapo na yeye mwenyewe akajisalimisha kwa uongozi wa Serikali ya kijiji na baadaye kupelekwa polisi.

Aliongeza kuwa, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani ili sheria iweze kuchukua mkondo wake baada ya uchunguzi kukamilika

SAMATTA AIPELEKA GENK EUROPA LEAGUE


Tarehe May 29, Mbwana Samatta ameandika historia mpya kwenye maisha yake baada ya kuisaidia timu yake ya Genk kushinda mchezo wa fainali ya play off na hatimaye kufuzu kucheza michuano ya Ulaya (Europa League).
Samatta ambaye alianza kwenye kikosi cha kwanza cha Genk ameisaidia klabu yake kupata ushindi wa magoli 5-1 kwenye uwanja wao wa nyumbani (Cristal Arena) dhidi ya Sporting Charleroi.

Alhamisi, 19 Mei 2016

DOLA ZA KIMAREKANI BILIONI 3 KUTUMIKA KUANZISHA MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage (kushoto) akiongea na Waandishi wa Habari (hawako pichani) kuhusu kuanza kwa mradi wa Mgodi wa kuchimba chuma na makaa ya mawe Liganga na Mchuchuma leo mjini Dodoma 19 Mei, 2016. Katikati ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge inayosimamia viwanda, biashara na uwekezaji, Mhe. Dkt. Dalaly Kafumu pamoja na Mkurugenzi Mwendeshaji toka Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Bwana Mlingi Mkucha.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge inayosimamia viwanda, biashara na uwekezaji, Mhe. Dkt. Dalaly Kafumu (kulia) akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wa Habari (hawako pichani) kuhusu kuanza kwa mradi wa Mgodi wa kuchimba chuma na makaa ya mawe Liganga na Mchuchuma leo mjini Dodoma 19 Mei, 2016. Kushoto ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage.


Na Benedict Liwenga, MAELEZO, Dodoma.

JUMLA ya dola Bilioni 3 za Kimarekani zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa Mgodi wa Makaa ya Mawe na Chuma wa Liganga na Mchuchuma.Kauli hiyo imetolewa Leo mini Dodoma na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage wakati akiongea na Waandishi wa habari mini Dodoma.

Jumatatu, 16 Mei 2016

Lidege likubwa zaidi duniani latua Australia

Antonov An-225 Mriya ndiyo ndege refu na nzito zaidi kuwai kujengwa.
Maelfu ya watu nchini Australia wanaopenda ndege walikusanyika kutizama ndege kubwa zaidi duniani ya Antonov An-225 Mriya, ilipowasili mjini Perth nchini humo.
Ndege hiyo yenye urefu wa mita 84 na uzito wa tani 175 bila ya kubeba mzigo wala mafuta, ilikuwa ikisafirisha jenereta yenye uzito wa tani 117.

KITISHO CHA BOMU CHAAHIRISHA MECHI YA MAN U

 
 Hofu ya kuwepo bomu uwanjani imesababisha mechi ya Manchester United na Bournemouth kuahirishwa.

Mechi ya mwisho katika ligi ya soka ya uingereza, EPL, kati ya Manchester united na Bournemouth imeahairishwa kufuatia wasiwasi wa bomu, uwanjani Old Trafford.