SHEKHE AUAWA KATIKA FUMANIZI
JESHI la Polisi Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma, linamshikilia mkazi wa Kijiji cha Likweso, Tarafa ya Mchoteka, Ally Mchumwa
kwa tuhuma za mauaji ya Shekhe wa kijiji hicho.
Kamanda
wa Polisi mkoani humo, Zubery Mwombeji, alisema tukio hilo limetokea
Mei 22, mwaka huu, baada ya mtuhumiwa (Mchumwa), kumfumania akifanya tendo la ndoa na mkewe.
"Mauaji haya yametokea saa tatu
asubuhi wakati marehemu ambaye amefahamika kwa jina la Seleman Mwalabu
(45), mtuhumiwa na mkewe Mariamu Husein, wakisaidiana kuvuna njugu
shambani.
"Wakati wakiendelea na kazi hiyo, mtuhumiwa alitoka
kidogo na kumuacha marehemu pamoja na mkewe wakiendelea na kazi hiyo,
aliporejea hakuwakuta shambani hivyo akashtuka," alisema.
Kamanda
Mwombeji alisema wakati mtuhumiwa akiwa katika kwenye sintofahamu hiyo,
alisikia sauti ikitoka porini jirani na shamba lake hivyo aliamua kwenda
na kumkuta mkewe na mtuhumiwa wakiwa uchi wa mnyama ikiashiria wametoka
kufanya tendo la ndoa.
Kutokana na hali hiyo, mtuhumiwa
alichomoa kisu na kumchoma nacho marehemu shingoni, kufariki papo hapo
na yeye mwenyewe akajisalimisha kwa uongozi wa Serikali ya kijiji na baadaye
kupelekwa polisi.
Aliongeza kuwa, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani ili sheria iweze kuchukua mkondo wake baada ya uchunguzi kukamilika
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni