Wanafunzi 14
walioongoza katika matokeo ya mtihani wa mwisho katika jimbo la Bihar
nchini India watalazimika kufanya tena mtihani kufuatia madai kwamba
walihusika na udanganyifu, serikali ya jimbo hilo imsema.
Uamuzi
huo uliafikiwa baada ya mmoja ya wanafunzi hao Ruby Rai mwenye umri wa
miaka 17 kuviambia vyombo vya habari kwamba sayansi ya siasa inahusisha
kupika.Kanda ya Video ya mahojiano hayo na yale ya wengine ilisambazwa sana. Mwaka uliopita, wazazi wa wanafunzi katika jimbo hilo walipigwa picha wakipanda kuta za shule ili kutoa majibu kwa wanafunzi wanaokalia mtihani.
Serikali ya jimbo hilo ilikuwa imetangaza hatua kali kama vile faini na vifungo jela kwa lengo la kuangamiza uovu huo mwaka uliopita.
Alama za chini zilizopatikana katika matokeo yaliotangazwa wiki iliopita zilichukuliwa kama ishara kwamba hatua zilizochukuliwa zimefanikiwa.
Hiyo ni hadi kanda ya video ya Ruby Rai ilivyopeperushwa hewani.
Serikali imesema kuwa matokeo yake na yale ya Saurabh Shrestha ambaye alikuwa wa kwanza katika somo la sayansi na alishindwa kujibu swali rahisi la somo la kemia yamepigwa marufuku mara moja
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni