Wakili wa China aliyepigwa na kuchaniwa nguo akitoka mahakamani
Mawakili wengi wa
China wamenyanyaswa, kukamatwa na hata kufungwa jela lakini picha ya
mmoja wao aliyekuwa na nguo zake zilizochanwa na maafisa wa polisi
imevutia hisia nyingi nchini China.
Yeye na mawakili wengine waliwaambia maafisa wa mahakama kwamba alishambuliwa na maafisa watatu katika mahakama moja mbele ya majaji wawili ambao walikataa ombi lake la kutaka kuanzisha kesi katika mahakama ya wilaya ya Nanning Mkoani Guangxi.
Bw Wu alipewa nguo nyengine lakini alijua uwezo wa kile alichokuwa akipanga kukifanya.''Asante alisema''.
Wakili huyo baadaye alitembea kupitia mlango wa mbele akiwa amebeba nakala zake za mahakamani akiwa na kalamu iliowekwa katika mfuko wa shati liliposuliwa.
Baadaye alipigwa picha nje ya jengo hilo la mahakama na picha hiyo kusambazwa. Hii ilikuwa na maana ya kutuma ujumbe kewa nchini China mawakili wananyanyaswa. Meseji sent
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni