Jumatano, 23 Novemba 2016

Mwanamume afariki shindano la kula kwa kasi Japan

Onigiri
Mwanamume nchini Japan amefariki siku tatu baada yake kusongwa na wali wakati wa shindano la kula kwa kasi.
Mwanamume mmoja, ambaye jina lake halijatolewa, alizimia wakati wa shindano hilo eneo la Hikone, Shiga mnamo 13 Novemba akijaribu kula matonge matano ya wali katika kipindi cha dakika tatu. Tonge la wali nchini Japan, kama lililo pichani, hufahamika kama Onigiri.
Alifariki siku tatu baadaye baada ya kukaa siku hizo zote akiwa hajapata tena fahamu, waandalizi wa shindani hilo wameambia vyombo vya habari Japan.
Mashindano ya kula chakula kwa kasi ni maarufu na huandaliwa mara kwa mara maeneo mengi Japan.
Wataalamu wanaonya kwamba kando na kusongwa na chakula, walaji huwa wamo hatarini ya kuharibu tumbo au koo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni