Mmarekani
asiyemtambua Mungu amewashtaki maafisa katika jimbo la Marekani la
Kentucky baada ya kukataliwa kuweka neno "IM GOD" ama '' MIMI NI
MUNGU'' badala ya namba za ya gari lake za usajili.
Bennie Hart
anasema nia ya kuweka maneno hayo kwenye pango la nambari ya gari lake
ni kuonesha kuwa inawezekana kumkosoa yeyote anayedai kuwa ni Mungu. Lakini wakuu wa uchukuzi katika jimbo hilo lenye kukaliwa na watu wenye imani kali za kidini wameamuru kuwa maneno hayo yanaweza kupoteza umakini wa madereva wengine na kwamba hayapendezi.
Wanaharakati wa uhuru wa kujieleza wamelivalia njuga suala hilo na sasa wanaunga mkono kesi ya Bwana Hart.
Anasema alikuwa na namnbari hiyo hiyo ya gari alipokuwa akiishi katika jimbo la Ohio kwa miaka 12 bila matatizo.
"Ninataka tu fursa sawa ya kuchaguza ujumbe wa mtu kwa ajili ya nambari ya usajili kama tu dereva mwingine yeyote yule ,"alisema Bwana Hart, anayeishi katika kaunti ya Kenton, Kaskazini mwa Kentucky.
" Hakuna matusi yoyote ama lugha isiyokubalika kuhusu maoni yangu kwamba imani za kidini zinategemea namna mtu binafsi anavyoelewa.
Muungano wa Marekani unaopigania uhuru wa kujieleza huko Kentucky (ACLU-KY) na wakfu wa uhuru wa kuabudu wamewasilisha kesi kwa niaba ya Bwana Hart dhidi ya katibu wa mamlaka ya uchukuzi ya jimbo Greg Thomas kuhusu uhuru wa kujieleza
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni