- Wanafunzi kadha wa shule moja eneo la Sichuan, China wamepata ngazi mpya kuwasaidia kupanda na kushuka urefu wa mita 800 kufika na kuondoka shuleni.
-
- Kijiji cha Atuler kimepewa jina la utani "kijiji cha mwamba". Kijiji hiki hupatikana mita 800 juu kwenye nyika eneo la Sichuan, China. Wanaoishi hapa ni watu wa jamii ya Yi, ambao pia hupatikana Vietnam na Thailand.
-
-
Hadi kufikia sasa, kulikuwa na ngazi 17 za mbao ambayo ilikuwa njia pekee ya wakazi wa kijiji hiki kutoka nje ya kijiji chao. Kupanda ngazi hizi lilikuwa jambo hatari na watu zaidi ya saba walifariki wakizikwea, wakazi wanasema.
-
Watoto karibu 20 kutoka kijiji cha Atuler husomea shule ya bweni, na ndipo waweze kufika hutakiwa kushuka kwa kutumia ngazi hiyo. Wakati wa likizo, shule zinapofungwa, hutakiwa kupanda ngazi tena kurejea kijijini.
-
- Sasa, ngazi ya chuma imejengwa kurahisisha safari yao. Lakini bado ni shughuli hatari, ingawa muda wanaotumia kupanda na kushuka umepungua.
-
- Watu wa jamii ya Yi wanaoishi Atuler wamekuwa wakikwea mwamba huo kwa miaka na mikaka na wana hata kanuni za kupanda. Wakati wa kupanda, wanaume wanawajibika kuwabeba na kuwatunza watoto. Watoto wa chini ya miaka 16 hawaruhusiwi kupanda au kushuka kwenye ngazi hiyo wakiwa peke yao.
-
Ngazi hiyo ya chuma ilijengwa
baada ya habari za kijiji hicho kugonga vichwa vya habari kimataifa
mwezi Mei. Ingawa wengi wanasifu ujenzi wa ngazi hiyo, wapo watu
wanaoshangaa ni kwa nini wanakijiji hao hawawezi kuhamia eneo
linalofikiwa kwa urahisi. Lakini wakazi waliambia wanahabari China
kwamba hawataki kuacha nyumba zao, hasa kuhamia mijini ambapo maisha
wanaamini ni magumu sana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni