Mwanamke mmoja
katika jimbo la Florida nchini Marekani, aliwafyatulia risasi wageni
waliokuwa wamemtembelea kwa sababu walikuwa wamekaa sana na walikuwa
wanapiga kelele, polisi wanasema.
Alana Annette Savell, 32,
alikuwa mwenyeji wa wageni hao wawili, wapenzi, katika jiji la Panama
pale walipoanza kupiga kelele sana.Polisi wanasema aliwaamrisha kuondoka kutoka nyumbani kwake, kabla ya kuwapiga risasi miguuni.
Walijipeleka hospitalini wakiwa na majeraha, ambayo hayakuwa mabaya sana.
Bi Savell ameshtakiwa kwa kuwashambulia watu akitumia bunduki.
Ofisi ya Mwendesha mashtaka wa wilaya ya Bay iliiambia BBC kwamba mwanamke huyo kwa jina Kristy Jo Mohr alikuwa amefika na mpenzi wake, ambaye walikuwa wamekutana kwenye baa, nyumbani kwa mshtakiwa mwendo wa saa saba usiku Jumatatu.
Bi Savell aliiambia polisi alianza kukerwa na wageni hao baada yao kuanza kunywa pombe na kuzungumza kwa sauti ya juu.
Baada ya kuwadokezea kwamba alikuwa amechoshwa nao kwa kula miayo au kuweka vyombo vya jikoni kwenye mashine ya kuosha vyombo, alichomoa bunduki yake na kuwafyatulia risasi miguuni.
Bi Mohr aliumizwa miguu yote miwili naye mpenzi wake, aliyetambuliwa tu kwa jina Cowboy akaumia mguu mmoja.
Bi Mohr ameambia polisi anakadiria kwamba kwa jumla Bi Savell alifyatua risasi nane au tisa.
Aliposhtukia amepigwa risasi mguuni, anasema alikimbia na kuingia kwenye gari.
Mpenzi wa washukiwa ameambia maafisa wanaochunguza kisa hicho kwamba alikuwa amemshauri kwamba mgeni akikatalia nyumbani baada ya kumwambia mara tatu, achukue bunduki na kufyatua risasi sakafuni.
"Hilo lisipofanya kazi, basi awafyatulie risasi miguuni," maafisa wa mashtaka wamesema.
Bi Savell kwa sasa bado anazuiliwa uchunguzi zaidi ukiendelea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni