Waziri mkuu wa
jimbo la Telangana nchini India amezua hisia baada ya kuhamia katika
nyumba mpya inayogharimu walipa kodi dola milioni 7.3.
Jumba hilo lina ukubwa wa mita 9,000 mraba katika mji wa Hyderabad.Jumba hilo lina vyoo vilivyo na uwezo wa kukinga risasi kuingia, ukumbi ulio na viti 250 na eneo la mikutano linaloweza kuingiza watu 500.
Jumba hilo lilibarikiwa na mshauri wa maswala ya kidini wa waziri huyo huku choo hicho kinachoweza kuzuia risasi kuingia kikifanyiwa masikhara.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni