Muungano wa
wanasheria nchini Gambia umesema kuwa kitendo cha Rais wa nchi hiyo
Yahya Jammeh kukataa matokeo ya kura zilizoonyesha kuwa ameshindwa
katika uchaguzi uliopita ni kuisaliti nchi hiyo.
Muungano huo umeitisha maandamano kwa nchi nzima mpaka pale Jammeh aliyeangushwa katika uchaguzi huo akabidhi madaraka.Hapo awali Jammeh alikubali kushindwa na kuahidi kuondoka madarakani lakini aliyakataa matokeo hayo siku ya Ijumaa.
Ujumbe wa wakuu wa nchi za Afrika unatarajiwa kusafiri kuelekea Gambia siku ya Jumanne kwa lengo la kuzungumza na Jammeh ili kuachia madaraka.
Marekani imeonya kuwa nchi hiyo inapitia katika mazingira magumu huku baadhi ya viongozi wa kijeshi wakitajwa kumuunga mkono Jammeh.
Ujumbe wa wakuu wa nchi za Afrika unatarajiwa kuwajumuisha Rais wa Nigeria, Ghana, Liberia na Siera Leone.
Kwa upande wake Baraza la usalama la umoja wa mataifa linajadili namna ya kutatua mgogoro huo leo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni