Jumamosi, 28 Januari 2017

APOTEA NJIA NA KUENDESHA BAISKELI KWA SIKU 30

Mwanamume huyo alisimamishwa baada ya kuendesha baiskeli kwa siku 30

Mwanamume mmoja nchini China ambaye alikuwa na matumaini ya kuendesha baiskeli hadi nyumbani kwao kusherehekea mwaka mpya, aligundua baada ya siku 30 kuwa alikuwa amepotea njia.
Mwanamume huyo alikuwa na matumaini ya kuwasil nyumbani kwao huko Qiqihar mkoa wa Heilongjian baada ya kuanzia safari yake huk Rizhao umbali wa kilomita 1,700.
Lakini alisimamishwa na polisi wa trafiki akiwa amepotea umbali wa kilomita 500 katika mkoa wa Anhui.
Wakati waligundua, polisi walimlipia tikiti ya treni ili arudi nyumbani.
Ripoti zinasema kwa mwanamume huyo alikuwa akilala maduka ya intaneti kwa sababu hakuwa na pesa.
Mwanamume huyo hakuwa na uwezo wa kusoma ramani na hivyo alikuwa akitegemea watu kumuelekeza.
Polisi walimsimamisha kwa sababu alikuwa akitumia barabara ambayo baiskeli haziruhisiwi barabarani.
Baada ya kugundua makosa yake, polisi na watu wote waliokuwa kituoni ambapo alisimama walichanga pesa na kumnunulia tikiti ili asafiri nyumbani

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni