Jumanne, 3 Januari 2017

Brazil: Wafungwa 55 wauawa katika vurugu

 Ulinzi uliimarishwa baada ya tukio hilo
Ulinzi uliimarishwa baada ya tukio hilo
Maafisa nchini Brazil wanasema wafungwa 55 wamepoteza maisha katika vurugu zilizotokea katika gereza moja nje ya mji wa Manaus.
Vurugu hizo katika gereza la Anisio Jobim zilianza siku ya Jumapili na kuisha baada ya saa kumi na saba pindi wafungwa hao waliposalimu amri.
Baadhi ya miili imekatwa vichwa huku mingine ikiwa imechomwa moto.
Mkuu wa usalama katika jimbo la Amazonas, Sergio Fontes, amewaambia waandishi wa habari kuwa vurugu hizo zilikuwa zimepangwa muda mrefu.
"kila kitu kinaashiria kwamba vurugu zilizotokea zilikuwa zimepangwa muda mrefu.

   Idadi kubwa ya wafungwa waliotoroka walikamatwa
Idadi kubwa ya wafungwa waliotoroka walikamatwa
Wafungwa waliweka bayana kwa uongozi wa gereza kwamba kila kitu kitakuwa sawa katika msimu huu wa sikukuu.
Hawakutekeleza ahadi yao, lakini Jee unaweza kuwaamini wahalifu?" Laa Hasha
Fontes ameongeza kusema kuwa baadhi ya wafungwa walitoroka na wengine wameuawa.
Hata hivyo, Idadi kubwa ya wafungwa waliokuwa wametoroka tayari wamekamatwa.
Nako nje ya gereza, ndugu wa wafungwa waliokusanyika walijawa na shauku ya kutaka kujua hali ya ndugu zao.
Mama wa mmoja ambae mwanae ni mfungwa ameonekana akishikilia gamba la risasi huku akisema polisi hawana nia ya kuwalinda wafungwa.
Maafisa wa gereza wanasema makundi hasimu yaliyopo nje na ndani ya gereza yamepigana kwa kutaka kuwa na sauti dhidi ya kundi jingine.
 
Ndugu na jamaa wakiomboleza nje ya gereza
Ndugu na jamaa wakiomboleza nje ya gereza
Wajumbe wa moja wapo ya makundi hayo, wametengwa katika magereza mengine.
Nae waziri wa katiba amekwenda katika gereza hilo ili kuangalia uwezekano wa kuhamishwa kwa baadhi ya wafungwa katika gereza jengine.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni