Jumanne, 3 Januari 2017

Abiria wamripoti Rubani mlevi kabla ya ndege kuondoka, Watanzania je?

Ndege hiyo ilitarajiwa kusafiri kutoka uwanja wa ndege wa Calgary Canada kuelekea nchini Mexico

Polisi huko Canada wamemkamata rubani mmoja aliyekuwa ndani ya ndege ya abiria kwenye chumba cha marubani akiwa amelewa chakari kwa mujibu wa vipimo alivyofanyiwa.
Rubani huyo alikuwa amepangiwa kuendesha ndege hiyo kwa safari ya kutoka uwanja wa ndege wa Calgary Canada hadi nchini Mexico ndipo lakini wafanyakazi wenzake wakamuona hakuwa katika hali sawa na kupiga ripoti.
Kisha punde baadae akaanguka na kuzirai.
Sasa amefunguliwa mashtaka ya kutaka kuendesha ndege akiwa mlevi na utovu wa nidhamu kazini.
Baadae rubani mwengine aliendesha ndege hiyo ya shirika liitwalo Sunwing iliyokuwa inaelekea Cancun mjini Mexico, ikiwa na abiria zaidi ya 100. 
Swali la kujiuliza ni Je kwa nini watanzania hawatoi taarifa ya madereva wa vyombo vya moto wanaokuwa wamelewa? na Je maji wanayokunywa madereva wakiwa safarini ni maji au pombe kali?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni