Ndege nchini India
zitakazoangusha kinyesi cha binaadamu kutoka angani zitapigwa faini ya
Rupee 50,000 sawa na dola 736 mahakama imeamuru.
Mtu mmoja
amelalama kwamba ndege zimekuwa zikiangusha uchafu huo kutoka chooni
juu ya makazi ya watu karibu na uwanja wa ndege wa Delhi. Vyoo vya ndege huweka uchafu wa chooni katika matangi maalum.
Matangi hayo hufunguliwa na uchafu huo kumwaga ndege inapotua.
Lakini mamlaka ya anga imekiri kwamba mtiririko wa uchafu huo hutokea angani ni kwa bahati mbaya.
Mahakama sasa imeagiza shirika hilo la usafiri wa ndege kuhakikisha kuwa kwamba ndege haziangushi kinyesi cha binadamu kutoka anagani wakati inapotua ama mahala popte karibu na uwanja wa ndege.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni