Jumanne, 3 Januari 2017

Ndugu wawili wakutana baada ya miaka 40

Ndugu wawili wakutana katika kituo cha kuwatunza wazee, baada ya kupoteana kwa zaidi ya miaka 40. Unaapoisikia habari hii kwanza utafikiri imetungwa makusudi wakati huu wa X-Mas kwa jinsi inavyosisimua
Deutschland Zwei Schwestern finden sich nach 40 Jahren im Altersheim wieder (picture-alliance/dpa/R. Priebe) Ndugu wawili wakutana baada ya miaka 40 katika nyumba ya wazee

Lakini si hadithi ya kubuni ni tukio la kweli tena lililotokea Desemba sita iliyopita-wenyewe Ujerumani wanaiita siku hiyo kuwa ni siku ya Nikolaus. Siku hiyo ya Desemba sita mnamo saa za usiku, Hedwig Horsch amekaa pamoja na wazee wenzake katika meza wakisubiri chakula cha usiku-mbele yake kulikuwa na bibi mmoja. Macho ya Hedwig hayakutulia yalimwandama bibi yule ambaye ni mgeni katika kituo chao cha kuwatunza wazee. Hedwig hakuweza tena kuvumilia, akapiga moyo konde na kumwendea yule bibi na kumuuliza anaitwa nani. Hapo hajawa na shaka yoyote: Mbele yake ameketi dadaake, Annelore ambae alifikiri amepotea-walionana kwa mara ya mwisho miaka 40 iliyopita MAMBO HAYO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni