Alhamisi, 27 Aprili 2017

Kisiwa chenye Wanaume wanaotafuta wanawake kutoka mataifa mengine

 Wanaume wanatafuta wanawake kutoka mataifa mengine
Athaya Slaetalid na mumewe Jan pamoja na mwana wao Jacob
Kuna upungufu wa wanawake katika kisiwa cha Faroe.
Hivyo basi wanaume katika kisiwa hicho wanatafuta wanawake kutoka maeneo mengine kama vile mataifa ya Thailand na Ufilipino.
Lakini je ni changamoto gani zinazowakumba wanawake wanaoelekea katika kisiwa hicho.
Wakati Athaya Slaetalid alipoelekea katika kisiwa hicho ambapo kipindi cha majira ya baradi huchukua muda wa miezi sita alikuwa akikaa karibu na kikanza ama heater kwa jina la Kiingereza kwa siku nzima.
''Watu walikuwa wakiniambia niende nje kwa sababu kuna jua lakini nilisema'': ''Hapana niacheni, nahisi baridi sana''.

Kuhamia katika kisiwa hicho miezi sita iliopita ilikuwa vigumu kwa Bi Athaya aliyekiri.
Alikutana na mumewe Jan alipokuwa akifanya kazi na rafikiye mmoja wa kisiwa hicho ambaye alikuwa ameanza biashara nchini Thailand.
Jan alijua mapema kwamba kumpeleka mkewe katika utamaduni huo, hali ya hewa itakuwa changamoto kubwa.
  Kisiwa cha Faroe chenye upungufu wa wanawake
Kisiwa cha Faroe chenye upungufu wa wanawake
"Nilikuwa na wasiwasi kwa sababu kila kitu alichokiacha nchini Thailand kilikuwa tofauti na kile alichokuja kuona katika kisiwa cha Faroe'', alisema.
''Lakini kwa sababu namjua Athaya nilijua ataingiliana na hali ya hewa''.
Kufikia sasa kuna takriban wanawake 300 kutoka Thailand na Ufilipino wanaoishi katika kisiwa cha Faroe.
Haionekani kuwa idadi kubwa lakini kisiwa hicho chenye idadi ya watu 50,000 sasa wanawakilisha watu walio wachache katika visiwa hivyo 18 kati ya Norway na Iceland.
Katika miaka ya hivi karibuni visiwa vya Faroe vimepata upungufu wa idadi ya watu huku vijana wakiondoka ili kutafuta elimu na huwa hawarudi.
Wanawake wameamua kuishi ughaibuni.

Upinzani kutangaza mgombea wake Kenya

Viongozi watano wa muungano wa upinzani Kenya (NASA)

 Viongozi watano wa muungano wa upinzani Kenya (NASA)
Muungano wa vyama vya upinzani nchini Kenya unatarajiwa kumtaja atakayewania urais dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti.
Tangazo hilo litafanyika huku nchi hiyo ikimaliza shughuli kura za mchujo za vyama, ambazo zimekumbwa na vurugu na madai ya kuiba kura.
Maelfu ya wafuasi wa upinzani wamefika katika uwanja wa Uhuru Park kuhudhuria mkutano huo.
Huku zikiwa zimesalia siku 102 tu kabla ya uchaguzi, muungano mkuu wa upinzani Kenya ulikuwa na muda mdogo kumtaja kiongozi wao. Muungano huo wa National Super Alliance, yaani NASA, una wanaume watano wote wanaotaka kuongoza, lakini inatarajiwa kuwa jopo litamchagua Raila Odinga.
Vigogo wengine kwenye muungano huo ni makamu wa rais wa zamani Kalonzo Musyoka, makamu wa rais wa zamani Musalia Mudavadi, waziri wa zamani wa mambo ya nje Moses Wetangula na mwenyekiti wa zamani wa baraza la magavana Isaac Ruto.
Bw Ruto, anayeongoza chama cha Chama cha Mashinani (CCM) alikuwa kwenye muungano wa vyama vinavyomuunga mkono Bw Kenyatta kabla ya kuhama na kuunda chama chake.
Bw Odinga ndiye kiongozi wa chama cha ODM, ambacho kina wabunge wengi zaidi katika Bunge la sasa.
Iwapo atachaguliwa kuwa mwaniaji wa NASA, basi itakuwa ni mara ya nne kwake yeye kupigania urais.
Kiongozi huyo bado anasisitiza kuwa alishinda uchaguzi wa mwaka 2007 ambapo rais wakati huo, Mwai Kibaki alitangazwa mshindi, na kuzua tafrani nchini Kenya ambapo watu zaidi ya elfu moja waliuawa.
Huku hayo yakijiri, wanasiasa wengi wanaendelea kupoteza viti vyao kwenye kura za mchujo.
 
Wafuasi wa chama cha Wiper chake Bw Kalonzo Musyoka
Wafuasi wa chama cha Wiper chake Bw Kalonzo Musyoka
 
Wafuasi wa chama cha ODM uwanjani Uhuru Park
Wafuasi wa chama cha ODM uwanjani Uhuru Park
  Bw Musyoka, Bw Odinga na Bw Wetangula
Bw Musyoka, Bw Odinga na Bw Wetangula
Wakenya kwenye mtandano wamekuwa wakiendesha kampeni inayoitwa Opresheni Fagia Wote, na mwandishi wetu Ferdinand Omondi anaripoti anasema huenda wanafanikiwa.
Baadhi ya maeneo ya uchaguzi yamemfuta kazi Gavana, Seneta, wabunge na madiwani wote.
Kampeni ya Fagia Wote inapania kuonyesha ghadhabu ya Wakenya kwa jinsi taifa hilo limeendeshwa kwa miaka minne iliyopita. Kumezuka vurugu kwenye sehemu kadhaa nchini na pia madai ya kuiba na kununua kura.

Askofu mmoja wa kike, Margaret Wanjiru ambaye amewahi kuwa waziri, ambaye kwa sasa alikuwa anawania kuwa Gavana mpya wa Nairobi, alilala kwenye seli ya Polisi alipokamatwa jana kwa madai ya kuzua rabsha katika kituo cha uchaguzi.
Kura za mchujo zinafaa kumalizika Jumapili.
Uchaguzi mkuu utafanyika tarehe 8 Agosti.

Arsenal, Tottenham zashinda Epl

Spurs

Mfungaji wa bao la Spurs kiungo Christian Eriksen
Mshike mshike wa kuwania ubingwa wa ligi kuu England umeendelea kushika kasi ambapo Tottenham Hotspur walipata ushindi ugenini wa bao 1-0 dhidi ya Crystal Palace.
Bao pekee la Spurs katika mchezo huo lilifungwa na kiungo Christian Eriksen, katika dakika ya 78 ya mchezo na hivyo kuendelea kuwakimbiza vinara wa ligi hiyo Chelsea, wanaongoza ligi kwa alama 78 huku Spurs wakiwa nafasi ya pili kwa alama 74.
  Arsenal
Beki wa Arsenal Nacho Monreal akishangalia
Nao washika mititu wa London Arsenal, walipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Leicester City, bao la kujifunga la beki wa Leicester Robert Huth, ndio liliwapa vijana wa Wenger alama tatu muhimu na kusogea mpaka nafasi ya sita katika msimamo wa ligi.
Vibonde wa ligi Middlesbrough wakautumia vyema uwanja wa nyumbani wa Riverside kuwa kuwachapa kwa bao 1-0 vibonde wengine wa ligi Sunderland ambao ndio wanaburuza mkia katika ligi hiyo

Barca, Madrid zapeta La Liga

Barca

Messi akifunga bao lake la 501 kwa Barcelona
Miamba ya soka la Hispania vilabu vya Barcelona na Real Madrid vimendelea kutamba katika ligi hiyo kwa kupata ushindi wa mabao mengi katika michezo yao.
Barcelona waliichapa timu inayoburuza mkia katika ligi Osasuna, kwa mabao 7 -1 mabao ya Barca yakifungwa na Lionel Messi aliyefunga mabao mawili, Andre Gomes, nae akafunga mawili kinda Francisco Alcacer, akatupia nae magoli mawili huku Javier Mascherano, akifunga bao moja.
   Real
wachezaji wa Real Madrid wakipongezana
Real Madrid wakiwa ugenini katika dimba la Municipal de Riazor, waliwafunga Deportivo La Coruna, kwa mabao 6-2, mabao ya Real yalifungwa na James Rodriguez, aliyefunga mara mbili na mengine yakifungwa na Alvaro Morata, Lucas Vazquez, Isco na kiungo Casemiro
Leganes wakashinda kwa 3 - 0 dhidi ya Las Palmas, Nao Valencia wakalala nyumbani kwa kufungwa 3-2 na Real Sociedad.