Alhamisi, 27 Aprili 2017

Arsenal, Tottenham zashinda Epl

Spurs

Mfungaji wa bao la Spurs kiungo Christian Eriksen
Mshike mshike wa kuwania ubingwa wa ligi kuu England umeendelea kushika kasi ambapo Tottenham Hotspur walipata ushindi ugenini wa bao 1-0 dhidi ya Crystal Palace.
Bao pekee la Spurs katika mchezo huo lilifungwa na kiungo Christian Eriksen, katika dakika ya 78 ya mchezo na hivyo kuendelea kuwakimbiza vinara wa ligi hiyo Chelsea, wanaongoza ligi kwa alama 78 huku Spurs wakiwa nafasi ya pili kwa alama 74.
  Arsenal
Beki wa Arsenal Nacho Monreal akishangalia
Nao washika mititu wa London Arsenal, walipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Leicester City, bao la kujifunga la beki wa Leicester Robert Huth, ndio liliwapa vijana wa Wenger alama tatu muhimu na kusogea mpaka nafasi ya sita katika msimamo wa ligi.
Vibonde wa ligi Middlesbrough wakautumia vyema uwanja wa nyumbani wa Riverside kuwa kuwachapa kwa bao 1-0 vibonde wengine wa ligi Sunderland ambao ndio wanaburuza mkia katika ligi hiyo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni